Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) limeeleza wasiwasi wake juu ya athari mbaya dhidi ya wanawake na wasichana zinazosababishwa na vurugu nchini Sudan, na kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Katika taarifa yake, mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Sima Bahous amesema, tayari wamepokea ripoti kuhusu uhalifu wa kijinsia na kingono, na kueleza wasiwasi wake kuwa, matukio hayo yataendelea kuongezeka kwa kasi zaidi.
Pia amesema UN Women inatoa woto kwa pande zote kuhakikisha kuwa hakuna mwanamke au msichana anayeathiriwa na uhalifu huu, na watendaji wote kuacha hatua za kuongeza hatari kama hizo.