Awamu ya nne ya mradi wa China wa kuchunguza Mwezi yaendelea hatua kwa hatua
2023-04-24 21:15:42| cri

Hivi karibuni, mhandisi mkuu wa mradi wa kuchunguza Mwezi wa China Bw. Wu Weiren alipozungumza na wanahabari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) ameeleza kuwa sasa kazi ya awamu ya nne ya mradi huo inaendelea hatua kwa hatua.

Kazi ya chombo cha kuchunguza Mwezi cha Chang'e-6 itatekelezwa mwaka 2024, ambayo ni pamoja na kukusanya sampuli za udongo katika upande wa mbali wa Mwezi na kuzirudisha hadi Duniani. Chombo cha Chang'e-7 kitaenda kwenye ncha ya kusini ya Mwezi ili kutafuta ushahidi wa kuwepo kwa maji huku kikifanya kazi pamoja na chombo cha Chang'e-8 kuunda kituo cha kimataifa cha utafiti wa kisayansi wa Mwezi na kufanya majaribio mfululizo juu ya uchunguzi na matumizi ya rasilimali za Mwezi.