Tanzania kuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya Ethiopia na kundi la waasi
2023-04-25 21:21:41| cri

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Jumapili alitangaza kuwa serikali yake iko tayari kuanza mazungumzo na kundi la waasi la Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA) nchini Tanzania, leo Jumanne, Aprili 25.

Haikuweza kufahamika mara moja ni wapi hasa mazungumzo hayo yatafanyika nchini Tanzania na ni pande zipi nyingine zinazohusika.

Abiy alisema serikali ya Ethiopia na watu watahitaji sana mazungumzo haya, na kutoa wito kwa kila mtu kubeba jukumu lake.

Waasi wa OLA wamekuwa wakipigana na serikali ya shirikisho ya Ethiopia tangu wagawanyike na Chama cha Ukombozi wa Oromo (OLF) mwaka 2018 kilipoachana na mapambano ya kutumia silaha.