Mjumbe wa China asema amani nchini Ethiopia ni ushindi wa umoja na majadiliano
2023-04-25 08:35:30| CRI

Mjumbe maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika Pembe ya Afrika, Xue Bing amesema, amani ya Ethiopia ni ushindi wa umoja na majadiliano.

Xue Bing amesema hayo baada ya kuhudhuria hafla iliyofanyika jumapili mchana mjini Addis Ababa, iliyolenga kutambua watu, makundi na serikali zilizochangia katika juhudi za amani nchini Ethiopia. Amesema mchakato wa amani nchini Ethiopia sio kwamba umeleta manufaa kwa amani na maendeleo katika Pembe ya Afrika, bali pia umetoa mfano halisi kwa maeneo mengine kutatua tofauti zao kwa njia ya amani.

Katika hafla hiyo, serikali ya Ethiopia ilitambua mchango wa China katika mchakato wa amani nchini humo.