Rais wa Kenya asema vifo vilivyotokana na imani ya dini ni ugaidi
2023-04-25 08:36:48| CRI

Rais wa Kenya William Ruto ametaja vifo vinavyohusika na imani ya kidini vilivyotokea katika mkoa wa pwani wa Kilifi ambapo polisi wamepata miili 47 na kuokoa watu waliodhoofu, kuwa ni ugaidi.

Rais Ruto ametoa maelekezo kwa mamlaka za usalama kufuatilia chanzo cha tukio hilo na kuchukua hatua zinazostahili baada ya polisi kupata watu waliofunga kula chakula mpaka walipokutwa na mauti, kufuatia maelekezo ya mchungaji wao.