Mjumbe wa China katika UM atoa wito wa kutekelezwa kihalisi utaratibu wa pande nyingi
2023-04-25 08:34:41| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito kwa nchi mbalimbali kutekeleza kihalisi utaratibu wa pande nyingi.

Balozi Zhang amesema hayo alipohutubia Mjadala wa Wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa na utaratibu wa pande nyingi.

Amesema hivi sasa jamii ya binadamu inakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kutokea hapo zamani, vitendo vya umwamba vitaleta athari mbaya kwa dunia, na makundi ya kisiasa yanazusha ufarakanishaji na mvutano mkubwa, hivyo umuhimu wa kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa unazidi kuongezeka.

Balozi Zhang amesisitiza kuwa, China, ikiwa nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama na nchi kubwa inayowajibika, inashikilia utaratibu wa pande nyingi, na itahimiza kikamilifu utekelezaji wa mapendekezo ya maendeleo, usalama, na ustaarabu duniani, kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China, na kushiriki kikamilifu kazi ya Umoja wa Mataifa, ili kuchangia katika kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa kimataifa, kukabiliana kwa pamoja changamoto na kulinda thamani ya pamoja ya binadamu wote.