Katibu mkuu wa UM akutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia
2023-04-25 19:23:06| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres tarehe 24 Aprili alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov.

Habari zimesema kuwa pande mbili zilijadili hali ya Ukraine na masuala mengine kuhusu Afghanistan na Syria.

Kuhusu Makubaliano ya usafirishaji wa bidhaa za kilimo kwa nje kwenye bandari ya Black Sea, Bw. Guterres alieleza wasiwasi wake juu ya vizuizi kwa kazi za kituo cha uratibu wa pamoja. Bw. Guterres aliwasilisha barua kwa rais Putin wa Russia kupitia Bw. Lavrov, akieleza mwelekeo wa kurekebisha, kurefusha na kupanua makubaliano hayo.