Guterres asema mfumo wa pande nyingi unakumbwa na shinikizo kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa UM
2023-04-25 20:22:35| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 24 Aprili lilifanya mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Kulinda pande nyingi zenye ufanisi kupitia kulinda kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa”, ambako katibu mkuu wa UM Bw. Antonio Guterres alisema mfumo wa pande nyingi unakumbwa na shinikizo kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa kwa Umoja huo.

Alisema kwa sasa hatua za pande nyingi zenye ufanisi zinahitajika zaidi katika kuzuia na kutatua mgogoro, kusimamia hali ya sintofahamu katika maendeleo ya kiuchumi, na kulinda malengo ya maendeleo endelevu. Ushirikiano wa pande nyingi ni kiini cha Umoja wa Mataifa, pia ni sababu ya kuwepo kwa UM na dhana ya mwongozo kwa umoja huo.

Aliongeza kuwa inapaswa kutafuta njia ya kusonga mbele na kuchukua hatua mara moja, ili kuzuia mgogoro na vurugu. Sasa ndio wakati wa kuhimiza ushirikiano, kuimarisha mashirika ya pande nyingi, na kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto za pamoja.