Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Baraza la Data Duniani
2023-04-25 08:37:02| cri


 

Rais Xi Jinping wa China jana ametuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa nne wa Baraza la data duniani la Umoja wa Mataifa.

Rais Xi amesema, maendeleo endelevu ni chaguo la lazima la jamii ya binadamu, na kutimiza maendeleo endelevu yenye nguvu na ya kijani ni matumaini ya pamoja ya watu wa nchi mbalimbali duniani. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kuimarisha ushirikiano wa data za kimataifa chini ya mfumo wa pendekezo la maendeleo ya dunia, na kusaidia utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.