Benki ya Dunia: Ongezeko la idadi ya wazee limezifanya nchi nyingi kutegemea zaidi wahamiaji
2023-04-26 21:08:40| cri

Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia tarehe 25 Aprili ilisema, idadi ya watu wanaozeeka inaongezeka kwa kasi kote duniani, hali ambayo inazifanya nchi nyingi zitegemee zaidi wahamiaji ili kutimiza ongezeko la watu kwa muda mrefu.

Ripoti hiyo ilisema nchi tajiri na nchi nyingi zaidi zenye mapato ya kati zinakabiliwa na suala la kupungua kwa idadi ya watu, hali ambayo inaharakisha zaidi ushindani wa dunia kwa wafanyakazi na wataalamu. Mbali na hayo, nchi nyingi zenye mapato ya chini zinakadiriwa kuwa na ongezeko kubwa la watu, na kuzifanya nchi hizo kuwa na shinikizo katika kuwapatia vijana nafasi zaidi za ajira.

Ripoti hiyo pia ilisema idadi ya wakimbizi imeongezeka kwa takriban mara mbili katika miaka kumi iliyopita. Ripoti ilisisitiza ulazima wa kusimamia wakimbizi, na kutoa wito wa kuwalinda wakimbizi na kupunguza hali ya watu kulazimika kukimbia makwao.