Watu milioni 6.6 nchini Somalia wanakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu licha ya mvua kunyesha
2023-04-26 08:38:54| CRI

Karibu watu milioni 6.6 nchini Somalia wanakabiliwa na mgogoro wa uhaba mkubwa wa chakula licha ya ongezeko la mvua linalotabiriwa na kupungua kwa bei ya chakula.

Tathmini iliyotolewa na Upambuzi wa Kina wa Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC) chini ya Umoja wa Mataifa imesema, kiwango cha uhaba wa chakula kitaendelea kuwa nchini Somalia mpaka mwezi Juni, huku asilimia 39 ya idadi ya watu nchini humo wakihitaji msaada wa dharura wa kibinadamu, licha ya kushuka kwa hatari ya baa la njaa katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa IPC, kiwango cha utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano bado ni kikubwa, ikikadiriwa kuwa watoto milioni 1.8 wanatarajiwa kuwa na utapiamlo kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka huu, wakiwemo watoto 477,700 wanaoweza kupata utapiamlo mkali.