China yapongeza maendeleo mazuri ya mchakato wa amani nchini Ethiopia
2023-04-26 08:37:26| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema, China inaipongeza serikali na watu wa Ethiopia kwa kufanikiwa kutatua migogoro ya ndani, utekelezaji wa mchakato wa amani unaoendelea vizuri.

Habari zinasema, serikali ya Ethiopia ilifanya mkutano wa kuthamini mchakato wa amani katika mji mkuu wa Addis Ababa. Katika mkutano huo, mjumbe maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika Pembe ya Afrika, Xue Bing, alipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Ethiopia kutokana na mchango wa China katika kutatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu nchini humo.