China yaweza kutumika kama mfano katika kutokomeza malaria barani Afrika
2023-04-26 08:38:16| CRI

Mtaalamu wa afya nchini Ethiopia amesema, nchi za Afrika zinaweza kuitumia China kama mfano bora katika kutokomeza malaria kwenye bara hilo.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua hivi karibuni, mtaalamu huyo, profesa mshiriki wa madawa katika Chuo Kikuu cha Ethiopia, Eyob Beyene amesema, kampeni ya China ya kupambana na malaria inaweza kutekelezwa kwa mafanikio katika nchi za Afrika, hususan nchini Ethiopia, kutokana na kufanana kwa hali ya hewa na tofauti ya idadi ya watu kati ya nchi hizo mbili. Amesema msaada wa China kwa Ethiopia katika kupambana na malaria umeongezeka tangu serikali ya China ilipopeleka timu ya kwanza ya wahudumu wa afya nchini humo, miaka zaidi ya 40 iliyopita.

Ameisifu serikali ya China kwa ujenzi wa Hospitali ya Tirunesh-Beijing pembezoni mwa mji wa Addis Ababa, Beyene ameeleza umuhimu wa Kituo cha Kukinga na Kutibu Malaria kilichojengwa kwa msaada wa China katika juhudi za Ethiopia za kupambana na ugonjwa huo.