Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 25 Aprili liliitisha mkutano wa dharura kuhusu hali ya Sudan.
Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun alitoa wito kwa pande mbili zinazozozana za Sudan kusimamisha vita mapema iwezekanavyo, na kutilia maanani mamlaka ya nchi na watu ili kuepuka kuchochea hali ya wasiwasi zaidi. Alisema China inaunga mkono kithabiti mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Sudan. China inataka Sudan isitishe vita mapema iwezekanavyo, na kurejea kwenye njia sahihi ya amani, utulivu na maendeleo ya nchi.
Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alitoa wito kwa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la UM na nchi za kikanda zishawishi pande hasimu nchini Sudan kusitisha mapambano mara moja ili kupunguza hali ya wasiwasi.