Watu 17 wauawa kufuatia milipuko iliyotokea kaskazini magharibi mwa Pakistan
2023-04-26 08:38:02| cri


 

Mkurugenzi wa Idara ya afya ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa nchini Pakistan amesema, watu 17 wameuawa wakiwemo askari polisi 9, raia 3 na wafungwa 5 na wengine 70 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea usiku wa jumatatu wiki hii katika ofisi ya idara ya kupambana na ugaidi ndani ya kituo cha polisi katika mkoa huo.

Polisi wamesema, idadi kubwa ya silaha na mavazi yaliyotengenezwa kwa ajili ya mashambulizi ya kujitoa mhanga zilihifadhiwa kwenye ghala za kituo hicho, na milipuko hii huenda ilitokea kwa bahati mbaya kutokana na uzembe wa wafanyakazi.