Sudan Kusini yasaini mpango wa kimkakati na WFP ili kujenga uwezo wa kujitegemea na kujiimarisha
2023-04-27 08:24:31| cri


 

Serikali ya Sudan Kusini na Shirika la Chakula Duniani (WFP) jana zimesaini mpango wa kimkakati wa miaka mitatu unaolenga kuisaidia nchi hiyo kujenga uwezo wa kujitegemea na kujiimarisha.

Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Kusini Bi. Mary Ellen McGroarty amesema, mpango huo unalenga kushughulikia ukosefu wa usawa na kutengwa kwa kupitia miradi yote ya WFP, ili kujenga jamii zilizoungana na zenye amani.

Naye Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, Deng Dau Deng amesema, katika miaka iliyopita, WFP imekuwa ikiiunga mkono Sudan Kusini kwa kusaidia juhudi za serikali ya nchi hizo za kupunguza uhaba mkubwa wa chakula.