Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Jean Kaseya ametoa wito kwa nchi za Afrika kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika bara hilo kupitia utoaji wa chanjo.
Katika taarifa yake, Kaseya amesema nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha kampeni za chanjo ili kukwepa kupunguza mafanikio yaliyopatikana kwa kuongeza juhudi za utoaji wa chanjo.
Amesema nchi za Afrika zinatakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayeachwa nyuma katika kupata chanjo, na kuongeza kuwa, katika muongo mmoja uliopita, chanjo zimeokoa maisha ya mamilioni ya watu, kuzuia magonjwa mabaya na milipuko ya magonjwa, na kupunguza gharama za huduma za afya.