Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kufikia makubaliano ya kusitisha vita haraka iwezekanavyo.
Balozi Zhang amesema hayo katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Sudan. Amesema, vita inayoendelea nchini Sudan imesababisha idadi kubwa ya vifo vya raia na uharibifu wa miundombinu. Amezitaka pande zote mbili katika mgogoro huo kutanguliza maslahi ya nchi na wananchi, kuhakikisha zinasitisha mapigano, kulinda raia ipasavyo, na kulinda usalama wa taasisi za kigeni, wafanyakazi na balozi za kidiplomasia nchini Sudan.