Kenya yazindua mradi wa kujifunza lugha ya Kichina kwa maofisa usalama
2023-04-27 08:28:39| CRI

Kenya imezindua mradi wa kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo (KDF) jana jumatano mjini Nairobi, na kuashiria hatua kubwa katika juhudi za kuimarisha uhusiano wa kitamaduni kati ya Kenya na China.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu msaidizi wa Idara ya Operesheni, Mipango, Nidhamu na Mafunzo wa KDF Fredrick Leuria amepongeza hatua hiyo, na kusema itaongeza uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na China kufikia ngazi mpya.

Naye Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian amesema, uzinduzi wa mradi wa kwanza wa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa maofisa usalama ni hatua kubwa katika kuimarisha uhusiano wa kirafiki na maelewano kati ya watu wa Kenya na China.