Msomi wa Australia ashambuliwa mtandaoni baada ya kusema “anataka kujionea hali ilivyo Xinjiang”
2023-04-27 21:02:00| CRI

Msomi wa Australia Bibi Maureen A Huebel hivi karibuni ameshambuliwa  mtandaoni na kufungiwa ukurasa wake binafsi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya kuonesha nia ya “kujionea hali ilivyo Xinjiang”.

Akihojiwa na mwanahabari kwa njia ya mtandao, Bibi Huebel amesema mashambulizi ya mtandaoni dhidi yake yanatokana na nia yake ya kutaka kufahamu hali halisi ya Xinjiang, na kwamba baadhi ya watu wanapenda kutunga uongo juu ya China ili kupotosha umma kuhusu taswira ya nchi hiyo, na wanaogopa kuwa utafiti wake utafichua uongo wao kuhusu Xinjiang.

Katika muda urefu uliopita, baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa wa Magharibi wamekuwa wakisambaza uvumi au taarifa potofu zinazodai kuwa kulikuwa na “mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa kabila la Wauigur huko Xinjiang”, lakini Bibi Huebel amesema ana mashaka makubwa juu ya madai hayo, kwa kuwa anajua ukweli kwamba pato la ndani la Xinjiang limekua kwa kasi, na idadi ya watu mkoani humo pia imeendelea kuongezeka. Ili kufahamu hali halisi, msomi huyo alifungua ukusara wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, na kwa muda mfupi tu akavutia maelfu ya wafuatiliaji.

Bibi Huebel amesema, mara nyingi aliitwa “muungaji mkono aliyeajiriwa wa China”, na kila mara alipotoa maoni chanya juu ya China, atalaumiwa kwa “kushindwa kuwa mfikiriaji mwenye uwezo wa kukosoa”.

Alipotangaza mpango wake wa kutembelea Xinjiang mwaka 2024 ili kufahamu kazi za kupunguza umaskini, mashambulizi makali na matusi mabaya zaidi yakaibuka dhidi yake.

Hata hivyo, Bibi Huebel amesema atatembelea miji mbalimbali ya Xinjiang pamoja na mume, binti na marafiki zake mwaka kesho kama alivyopanga, ili kuendeleza utafiti wake kuhusu kazi ya upunguzaji wa umaskini huko Xinjiang.

Bibi Huebel amesema baadhi ya wenzake wa Australia wana maoni tofauti naye kuhusu China, na anaona kuwa sababu yake ni kutoifahamu nchi hiyo “kutokana na upumbavu”.
Msomi huyo anaona China itakuwa msimamizi bora wa utaratibu wa dunia, na nchi zote zitanufaika nayo. Ametoa mwito kwa Australia kufuatilia upya “Karne ya Asia” na kutopoteza fursa hii kubwa. Bibi Huebel amesema, China sio tishio, bali ni fursa. Australia inapaswa kujiunga kwenye ushirikiano na China.