Marais wa China na Ukraine wazungumza kwa simu
2023-04-27 08:30:47| CRI

Rais Xi Jinping wa China amezungumza kwa simu na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambapo wamebadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya pande hizo mbili na mgogoro unaoendelea nchini Ukraine.

Akizungumzia suala la Ukraine, Rais Xi amesisitiza kuwa China siku zote inasimama katika upande wa amani, na kushikilia msimamo wa kuhimiza mazungumzo ya amani. Amesema China itatuma mjumbe maalumu kuhusu mambo ya Ulaya na Asia kufanya ziara nchini Ukraine, ili kufanya mawasiliano ya kina na pande mbalimbali kuhusu ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Kwa upande wake rais Zelensky amesisitiza kuwa, Ukraine inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kutumai kuanzisha ushirikiano na China katika pande zote, ili kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kujikita kwa pamoja katika kulinda amani na utulivu wa dunia.