Jeshi la Burkina Faso limesema, wanajeshi 33 wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulizi lililotokea jana dhidi ya kikosi cha kijeshi mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, kituo cha jeshi cha Ougarou kililengwa katika shambulio hilo lililotokea jana asubuhi, na kuongeza kuwa, mapigano yalikuwa makali na wanajeshi hao waliweza kuwakamata washambuliaji 40 kabla ya kuwasili kwa vikosi vingine.