China yachambua hali ya uchumi na kazi
2023-04-28 15:32:44| cri

Rais Xi Jinping wa China leo Ijumaa ameongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na kuchambua hali ya sasa ya uchumi na kazi za uchumi.

Mkutano huo unaona kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, mikoa na idara zote zimeratibu vyema hali mbili kuu za ndani na kimataifa, kuratibu vizuri hatua za kuzuia na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuratibu vizuri maendeleo na usalama. Aidha ukuaji wa uchumi umekuwa mzuri kuliko ilivyotarajiwa, mahitaji ya soko yanaimarika taratibu, maendeleo ya uchumi yanaonesha mwelekeo mzuri na kufufuka, na kazi za kiuchumi zikiwa na mwanzo mzuri.

Mkutano huo pia umebainisha kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi kwa sasa umekuwa wa kurejea, lakini nguvu ya ndani sio imara, mahitaji bado hayatoshi, mageuzi ya kiuchumi na uboreshaji vinakabiliwa na vizuizi vipya, na kukuza maendeleo yenye ubora wa juu bado kunahitaji kushinda ugumu na changamoto nyingi.