Tanzania, Rwanda zayapa uzito maswala ya biashara na uwekezaji
2023-04-28 22:26:11| cri

Tanzania na Rwanda zimekubaliana kufanya mageuzi katika sekta ya usafirishaji na usambazaji ili kuimarisha biashara na uwekezaji katika nchi hizo mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi mara baada ya kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema kiwango cha biashara kati ya nchi zao hakiakisi rasilimali nyingi zilizopo, hivyo kuna haja ya kutumia miundombinu kukabiliana na changamoto hiyo.

Kuhusu suala hilo, alisema lazima kuwe na mageuzi katika sekta hiyo ili nchi hizo mbili ziwe katika nafasi ya kutumia maliasili zilizopo.

Kwa upande wake, Paul Kagame wa Rwanda alisema kuwa Tanzania ni mshirika mkuu wa Rwanda hasa kwenye masuala ya usafirishaji na uunganishaji wa biashara.