Kenya yaomba msaada ili kutekeleza mipango yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2023-04-28 08:35:34| CRI

Kenya Alhamisi imetoa wito kwa washirika wake wa maendeleo dola za kimarekani bilioni 73.5 ili kuisaidia kutekeleza mipango yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi nchini humo Festus Ng’eno mjini Nairobi. Amesema Kenya, kama nchi nyingi zinazoendelea, iko hatarini sana kutokana na mabadiliko ya tabianchi na inahitaji msaada wa kutosha wa fedha ili kutekeleza hatua zake za kukabiliana na janga hilo.

Kenya kama nchi wanachama wengine wa Mkataba wa Paris, inatakiwa kuanzisha mpango wa utekelezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ili kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kukabiliana na athari za hali ya hewa, na kuufanyia marekebisho kila baada ya miaka mitano.