Zaidi ya wachina 1,300 waondolewa salama kutoka Sudan
2023-04-28 08:32:14| cri


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema, hadi kufikia sasa, zaidi ya raia 1,300 wa China wameondolewa salama kutoka Sudan.

Mao amesema, tangu mapigano yatokee nchini Sudan, serikali ya China imefanya juhudi kulinda usalama wa raia wa China kufuatia maelekezo yaliyotolewa na rais wa China, Xi Jinping, na kuanza operesheni ya kuwaondoa raia hao.

Mao amesema, kwenye operesheni ya uhamiaji, China pia iliwasaidia raia wa nchi nyingine tano kuondoka nchini Sudan kwa kutumia meli ya China.