China yajibu matamshi ya rais wa Korea ya Kusini kuhusu Mapambano ya Changjinhu
2023-04-29 17:45:51| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema ushindi wa China katika vita ya Korea dhidi ya Marekani ulithibitisha kuwa, nchi yoyote au jeshi lolote vikienda kinyume na mkondo wa kihistoria, na kuvamia nchi nyingine, hakika vitapigwa vibaya.

Rais wa Korea ya Kusini Yoon Seok-Youl ambaye yuko ziarani nchini Marekani amesema, vikosi vya Marekani vilipata ushindi mkubwa katika mapambano ya Changjinhu, wakati vilikuwa vikizingirwa na vikosi vya China katika vita ya Korea iliyotokea miaka ya 50 karne iliyopita.
Mao amesema, katika mapambano hayo, zaidi ya wanajeshi elfu 240 waliangamizwa, na hata kamanda mmoja alikufa katika ajali wakati wa kutoroka, na Marekani inaona kuwa ilikuwa safari ndefu zaidi ya jeshi la Marekani ya kutoroka baada ya kushindwa.