Watu wanne wafariki kutokana na kupasuka kwa bwawa nchini Yemen
2023-05-01 08:55:23| CRI

Watu wanne wamefariki nchini Yemen baada ya bwawa la Al-Aqabi lililoko katika jimbo la Al Mahwit kupasuka.

Mamlaka za huko zimethibitisha kuwa mafuriko yaliyosababishwa na kupasuka kwa bwawa hilo yamesomba msikiti mmoja, na watu wanne waliokuwa ndani yake wamepoteza maisha, huku nyumba za karibu pia zikiharibiwa.

Ofisa mmoja wa kundi la Houthi ambalo limedhibiti jimbo hilo tangu mwaka 2014, amesema kupasuka kwa bwawa hilo kumesababishwa na mvua kubwa na kazi za uokoaji bado zinaendelea.

Kituo cha hali ya hewa cha Yemen kimeonya raia walioko katika majimbo kadhaa ikiwemo Al Mahwit, kutosafiri kwenye maeneo yenye mafuriko, mabonde na miamba wakati na baada ya mvua kunyesha.