Pande zinazopambana nchini Sudan zimekubali kurefushwa muda wa kusitisha mapambano kwa saa 72
2023-05-01 08:35:54| CRI

Jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) wameahidi kuendelea kufuata makubaliano ya usitishaji vita mpya kwa muda wa saa 72 kuanzia saa sita usiku Jumapili.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Sudan imesema kutokana na juhudi na ombi la upatanishi wa Saudi Arabia na Marekani, wamekubaliana kurefusha muda wa usitishaji vita kwa saa 72 zaidi kuanzia mwisho wa muda wa sasa.

Kikosi cha msaada wa Haraka (RSF) kimesema katika taarifa yake kuwa ili kuitikiwa mwito wa ndani, kikanda na kimataifa, kinatangaza kurefushwa muda usitishaji wa mapambano kwa sababu za kibinadamu kwa saa 72 zaidi kuanzia usiku wa manane.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Sudan imesema kufungwa kwa anga ya nchi hiyo kutarefushwa hadi Mei 13, lakini safari za ndege kwa ajili ya misaada ya kibinadamu zitaruhusiwa baada ya kupata kibali kutoka kwa mamlaka husika na idhini ya jeshi la Sudan.

Hadi sasa mapigano nchini Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 500 na wengine zaidi ya 4,000 kujeruhiwa.