Tunisia yazuia majaribio 12 ya uhamiaji haramu
2023-05-01 09:09:49| CRI

Msemaji wa kikosi cha ulinzi wa pwani ya Tunisia Houcemeddine Jbabli, amesema Tunisia imezuia majaribio 12 ya uhamiaji haramu wa kuvuka bahari ya Mediterranean hadi pwani ya Italia.

Bw. Jbabli ametoa taarifa ikisema kikosi cha walinzi wa pwani cha Tunisia kimezuia majaribio hayo mwishoni mwa Ijumaa na mapema ya Jumamosi kutoka pwani za kusini, kaskazini na mashariki ya kati.

Kwenye operesheni hizo kikosi hicho kimewaokoa wahamiaji haramu 238 kutoka kwenye boti zilizozama. Tunisia iliyoko katikati ya bahari ya Mediterranean, imekuwa moja ya vituo maarufu vya usafiri kwa uhamiaji haramu unaoelekea Ulaya.