Mbunge wa Zimbabwe: Ufuatiliaji wa siri wa Marekani kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa haukubaliki
2023-05-02 14:21:27| CRI

Mbunge wa Zimbabwe ambaye pia ni waziri wa zamani wa teknolojia ya habari na mawasiliano na usalama wa mtandao Supa Mandiwanzira amesema Marekani siku zote inajidai kuwa inalinda hadhi na majukumu ya Umoja wa Mataifa, lakini imezusha “dhorura ya ufuatiliaji wa siri” katika Umoja wa Mataifa, na inapaswa kuwajibika kwa vitendo hivyo.

Mandiwanzira amesema kitendo cha hivi karibuni cha Marekani kufuatilia kwa siri nchi nyingi duniani na mashirika mengi ya kimataifa ikiwa ni pamoja na washirika wake kimefichuliwa, na kuzusha wasiwasi mkubwa na shutuma za jumuiya ya kimataifa. Mandiwanzira amesema Marekani inadukua mara kwa mara mambo ya mashirika ya kimataifa, ili kutumia ushawishi wake, na nchi nyingine duniani zinapaswa kuwa waangalifu, kwani Marekani inazingatia tu kujitafutia maslahi yake, ndio maana imeongeza uwekezaji wake katika idara za ujasusi na kumfuatilia kwa siri katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. Vitendo hivyo ya Marekani ni lazima vikemewe.