Wakati Zambia imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi, Rais wa nchi hiyo Hakainde Hichilema, amesisitiza umuhimu wa masikilizano kwenye sekta ya leba kwa ukuaji wa uchumi na ajira.
Rais Hichilema amesema itakuwa ni vigumu kubuni nafasi za ajira bila ukuaji wa uchumi ambao unaweza kuvurugika kutokana na migogoro kati ya waajiri na waajiriwa.
Rais Hichilema pia amesema kuimarishwa na kuboreshwa kwa mazingira ya waajiriwa, kunawezekana tu endapo biashara zitapata faida kwa ajili ya uwekezaji mpya.