China yaipongeza Uzbekistan kwa kupiga kura ya maoni ya katiba mpya kwa amani
2023-05-03 15:22:19| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeipongeza Uzbekistan kwa kupiga kura ya maoni ya katiba mpya kwa amani

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo imesema, China inaamini kuwa chini ya rais Shavkat Mirziyoyev, watu wa Uzbekistan watatimiza maendeleo zaidi katika nyanja zote katika juhudi za mageuzi na maendeleo ya nchi hiyo.

Pia Wizara hiyo imesema, China iko tayari kufanya kazi na Uzbekistan kuimarisha ushirikiano wa kina wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali, na inalenga kupata mafanikio mapya katika kujenga jamii ya pamoja ya China na Uzbekistan yenye hatma ya pamoja.

Uzbekistan ilifanya kura ya maoni siku ya Jumapili, ambayo imekubali marekebisho ya katiba ya nchi hiyo. Katiba hii mapya imeanza kutumika rasmi Jumatatu.