Wakati mapambano kati ya majeshi ya Sudan (SAF) na vikosi vya Jeshi la uungaji mkono wa haraka (RSF) yanaendelea, Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kuwa idadi ya watu waliouawa imeongezeka na kuwa zaidi ya 550, na idadi ya majeruhi imefikia 4,926.
Licha ya pande mbili kuridhia usitishaji wa mapigano kwa saa 72, mapigano kati ya pande hizo mbili yaliendelea katika maeneo mbalimbali ya miji ya Khartoum na Omdurman.
Wakati huo huo vyombo vya habari vimeripoti kuhusu mpango wa Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini wa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku saba. Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imesema katika taarifa yake kwamba kamanda wa jeshi la serikali ya Sudan Abdel Fattah Al-Burhan na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo wamekubali mpango huo.