China na Myanmar zakubaliana kuboresha ushirikiano wa kina wa kimkakati
2023-05-03 15:22:56| CRI

China na Myanmar zimekubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano wa kina wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano kati ya kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang uliofanyika katika mji mkuu wa Myanmar, Naypidaw.

Katika mkutano huo, waziri Qin Gang amesema, China imeweka umuhimu mkubwa katika uhusiano wake na Myanmar, na kwamba China inatarajia kuwa Myanmar itatimiza utulivu na maendeleo ya taifa. Ameongeza kuwa, China inaiunga mkono Myanmar katika kutafuta njia ya maendeleo yenye umaalum wa Myanmar inayoendana na mazingira halisi ya taifa hilo.

Kwa upande wake, kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing amesema, katika miaka karibu 70 tangu Myanmar na China zianzishe uhusiano wa kidiplomasua, nchi hizo zimedumisha kasi ya maendeleo na kupata mafanikio mazuri. Ameongeza kuwa, nchi yake iko tayari kufanya kazi na China ili kuboresha zaidi urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo, na kujenga kihalisi jamii ya binadamu ya Myanmar na China yenye mustakabali wa pamoja.