Katibu Mkuu wa UM aonya kuhusu “msukosuko mkubwa zaidi wa kibinadamu” unaoikabili Afghanistan
2023-05-03 08:28:03| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameonya kuhusu “msukosuko mkubwa zaidi wa kibinadamu” duniani unaoikabili Afghanistan na kutoa wito wa ufadhili zaidi kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na hali hiyo.

Bw. Guterres amesema hayo kwenye mkutano kuhusu suala la Afghanistan uliofanyika huko Doha, Qatar na kushirikisha wawakilishi kutoka nchi na mashirika zaidi ya 20, zikiwemo China, Russia na Marekani.

Amesema kwa sasa asilimia 97 ya watu nchini Afghanistan wanaishi katika hali ya umaskini ambapo theluthi mbili ya watu wake wanahitaji misaada ya kibinadamu kwa mwaka huu, lakini mpango wa misaada ya UM umepata ufadhili wa dola milioni 294 tu, ambazo ni pungufu kwa asilimia 94 ikilinganishwa na ilivyopangwa.