Jeshi la Sudan lakubali kurefusha usitishaji vita kwa siku 7 zaidi, licha ya mapambano kuendelea mjini Khartoum
2023-05-04 08:46:02| CRI

Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kukubaliana na mpango wa kikanda unaopendekeza usitishaji mapigano wa wiki moja ili kukomesha mapigano kati ya jeshi la serikali na vikosi vya msaada wa haraka (RSF).

Taarifa iliyotolewa na jeshi inasema ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kukabiliana na mgogoro wa sasa wa nchi hiyo, Shirika la Maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki (IGAD) lilitoa pendekezo jipya ikiwa ni pamoja na kurefusha muda wa kusitisha mapigano kwa wiki moja, na kumteua mwakilishi kutoka kila upande kujadili usitishaji wa mapigano.

Jeshi la Sudan limesema lina matumaini kuwa upande mwingine utazingatia matakwa ya makubaliano ya kusitisha mapigano. Hata hivyo vikosi vya msaada wa haraka (RSF) bado havijatoa tamko lolote kuhusu mpango huo wa IGAD.