Msomi wa Mali: Ujenzi wa nchi ya kisasa wenye umaalumu wa China una umuhimu wa kimataifa
2023-05-04 15:51:03| CRI

“Ujenzi wa nchi ya kisasa wenye umaalumu wa China” imekuwa dhana inayotajwa mara kwa mara kwenye jumuiya ya kimataifa. Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang kutoka nchini Mali Prof. Yoro Diallo hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema dhana hiyo ina umuhimu kwa dunia nzima, na inaweza kutoa ufumbuzi kwa changamoto mbalimbali zinazoyakabili maendeleo ya binadamu, na inastahili kuigwa na nchi zinazoendelea.

Prof. Diallo hivi karibuni alihudhuria Kongamano la Lanting (Lanting Forum) kuhusu “Ujenzi wa nchi ya kisasa wenye umaalumu wa China na Dunia” lililofanyika mjini Shanghai, na aliguswa sana na mjadala wa wageni kutoka nchi mbalimbali kuhusu dhana hiyo. Akimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Mamadou Tangara, anasema kwamba mafanikio ya China yamezitia moyo nchi nyingi zinazoendelea kwenye juhudi za kutafuta mipango ya kupunguza umaskini inayolingana na hali halisi ya nchi zao, ili kuhimiza maendeleo na ustawi kwa ufanisi. Prof. Diallo amesema, China, ambayo pia iliwahi kuwa nchi maskini, imekua hatua kwa hatua hadi kuwa nchi ya uchumi mkubwa wa pili, nchi ya kwanza kwa biashara ya bidhaa, nchi ya kwanza kwa akiba ya fedha za kigeni, nchi ya kwanza kwa viwanda vya utengenezaji bidhaa kote duniani, na pia imefanikiwa kujenga mifumo mikubwa zaidi ya elimu ya lazima, uhakikisho wa kijamii na huduma za afya duniani. China pia imetumia miongo kadhaa kukamilisha mchakato wa maendeleo ya viwanda ambao ulizichukua nchi za Magharibi karne kadhaa, mafanikio ambayo kweli ni ya kushangaza. Amesema nchi nyingi za Magharibi zimejiendeleza kwa njia za utumwa, ukoloni na unyonyaji dhidi ya nchi nyingine na watu wengine, lakini mafanikio ya China kujijenga kuwa nchi ya kisasa yamepatikana kwa kuwategemea Wachina wenyewe.

Prof. Diallo amesema, katikazaidi ya miaka 40 iliyopita tangu China ianze mageuzi na kufungua mlango, serikali ya China imefanikiwa kuwaondolea watu zaidi ya milioni 800 kutoka kwenye umaskini uliokithiri, kuwafanya watu zaidi ya milioni 400 wafikie daraja la kipato cha kati, hali ambayo inamaanisha kuwa ujenzi wa China ya kisasa unaleta ustawi wa pamoja kwa wananchi wote. Hali ya “tariji wazidi kuwa tariji, maskini wazidi kuwa maskini” sio ya kisasa, na mambo yale ya kisasa yanayohudumia mataifa machache na watu wachache pia sio ya kisasa. Prof. Diallo anaona, ustawi wa pamoja wa watu wote duniani, unahitaji maendeleo ya pamoja ya nchi na sehemu zote. Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia ndio bidhaa za umma zilizotolewa na China kwa jumuiya ya kimataifa, na pia ni majukwaa ya wazi yanayolenga kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja. Ujenzi wa mambo ya kisasa kwenye umaalum wa China utaleta haki zaidi kwenye usimamizi wa dunia, na kusukuma mbele nchi mbalimbali kuchangia kwenye ujenzi wa dunia iliyo bora zaidi.