Rais wa Kenya atoa mwito kurahisisha usafiri wa watu kuhimiza mafungamano ya kikanda
2023-05-04 09:08:11| CRI

Rais William Ruto wa Kenya amehimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD kuondoa vizuizi vya usafiri kwa watu, huduma na bidha, ili kuimarisha mafungamano ya kikanda.

Taarifa iliyotolewa na makao mkuu ya Jumuiya ya EAC huko Arusha Tanzania, imesema rais Ruto ametoa mwito huo katika uzinduzi wa ripoti kuhusu “Hali ya Uhamiaji katika Mashariki na Pembe ya Afrika” huko Nairobi.

Taarifa imesema rais Ruto ameona kuwa kuondolewa kwa vizuizi ni lazima kwa ukuaji na maendeleo endelevu katika eneo la mashariki na pembe ya Afrika.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa nchi wanachama katika kanda hiyo kuondoa vizuizi vya mipakani ambavyo vinakwamisha usafiri wa watu, bidhaa na huduma.