Ongezeko la uchumi wa Kenya kwa mwaka 2022 lapungua na kufikia asilimia 4.8
2023-05-04 21:56:00| cri

Idara ya Takwimu ya Taifa la Kenya (KNBS) imesema, uchumi wa Kenya kwa mwaka 2022 uliongezeka kwa asilimia 4.8, ikiwa ni chini ya kiwango cha asilimia 7.6 cha mwaka 2021.

KNBS imesema kupungua kwa kasi kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kulisababishwa na kudidimia kwa sekta mbalimbali zikiwemo kilimo na utengenezaji, na kuongezeka kwa mfumko wa bei.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mtazamo wa Uchumi kwa mwaka 2023 jijini Nairobi, Mkurugenzi mkuu wa KNBS Macdonald Obudho amesema, uhaba wa mvua ulisababisha mavuno duni ya bidhaa za kilimo mwaka jana, ikiwemo chai, kahawa, na mbogamboga.