Serikali ya Ethiopia na kundi la waasi la OLA wamaliza mazungumzo ya amani bila kufikia makubaliano
2023-05-04 09:19:57| CRI

Idara ya Mawasiliano ya serikali ya Ethiopia (EGCS) imesema duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA) imekamilika bila kufikia makubaliano.

Taarifa hiyo imesema ingawa mazungumzo hayo yamekuwa ya kiujenzi kwa kiasi kikubwa, kwa bahati mbaya hayajawezesha kufikiwa kwa makubaliano kuhusu baadhi ya masuala. Pande zote mbili zimekubali haja ya kuendelea na mazungumzo ili  kumaliza mgogoro kwa njia ya amani.

Idara hiyo pia imesema serikali ya Ethiopia inajitahidi kutafuta suluhu ya amani kwa mgogoro wa Oromia kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.