Uchunguzi waonesha kuwa Afrika ni kituo kikuu cha mauzo ya nje ya bidhaa za Kenya kwa mwaka 2022
2023-05-04 09:07:27| CRI

Idara ya takwimu ya Kenya KNBS, imesema Afrika ilikuwa kituo kinachoongoza kwa mauzo ya nje ya bidhaa za Kenya mwaka 2022, ikichangia asilimia 41 ya pato la jumla la mauzo ya nje ya nchi hiyo.

Idara hiyo imetoa takwimu za uchunguzi wa kiuchumi kwa mwaka 2023, ikisema thamani ya jumla ya mauzo ya nje ya bidhaa za Kenya kwa nchi za Afrika kwa mwaka jana ilifikia dola bilioni 2.62 za kimarekani, huku Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ikichukua asilimia 63 ya mauzo hayo.

Uchunguzi huo umesema Uganda bado inaongoza kati ya nchi za Afrika zinazonunua zaidi bidhaa za Kenya, ikichangia asilimia 11.1 ya mauzo ya nje ya nchi hiyo. Uchunguzi huo wa kila mwaka hutoa taarifa zinazohusiana na jamii na uchumi kwa kipindi cha miaka mitano.