Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amezindua Ajenda 2050 ya Nigeria (NA 2050) mjini Abuja, ambayo ni mpango mpya wa maendeleo ya muda mrefu unaolenga kuifikisha nchi hiyo kuwa nchi ya juu yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2050.
Rais Buhari amesema mpango huo unatarajia kuhakikisha Pato la Ndani kwa kila mtu kufikia dola za kimarekani 33,328 kwa mwaka, na pia una ruwaza ya kujenga uchumi wenye msukumo wa kiviwanda na unaotegemea ujuzi ambao unaweza kuhimiza maendeleo endelevu na shirikishi kwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa makaridio ya serikali, mchango wa uwekezaji katika Pato la Ndani la nchi hiyo utafikia asilimia 40.11 ifikapo mwaka 2050 ikilinganishwa na asilimia 29.40 ya sasa, huku idadi ya jumla ya ajira inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 203.41.