Benki Kuu ya Marekani yaongeza kiwango cha riba kwa alama ya robo ya asilimia
2023-05-04 22:52:52| cri

Benki Kuu ya Marekani imeongeza kiwango cha riba kwa alama ya robo ya asilimia hadi asilimia 5-5.25, ikisema inaendelea kuwa macho na hatari za mfumuko wa bei.

Ikiwa ni mara ya kumi kwa kuongeza kiwango cha riba tangu mwezi wa Machi mwaka jana, sera ya kubana matumizi ya fedha inalingana na matarajio ya soko.

Hata hivyo, bado kuna watu wengi ambao wametoa wito wa kusitisha kuongeza kiwango cha riba kufuatia mfumuko wa bei nchini Marekani kupungua katika siku za karibuni na hatari za kushuka kwa uchumi zikiongezeka.