WANAWAKE NA WATOTO KATIKA MACHAFUKO
2023-05-05 08:00:06| CRI

Hivi karibuni, jamii ya kimataifa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mapigano yanayoendelea nchini Sudan, na kutoa wito wa kumaliza mapigano hayo. Katika mazingira kama haya, waathirika wakubwa wanakuwa ni wanawake na watoto. Tumeona jinsi vita vinavyotenganisha familia, kusababisha wanawake na wasichana kufanywa watumwa wa ngono, kuandikisha watoto wa kiume katika makundi ya silaha kuwa wapiganaji, na mambo mengine kama hayo.

Bila kusahau wanawake wajawazito, ambao kama vita ikitokea, katika kukimbia mapigano, wanaweza kupoteza ujauzito au hata kujifungua sehemu ambazo si salama, na hivyo kuhatarisha maisha yao na mtoto. Jambo lingine ambalo linapaswa kufuatiliwa ni huduma za kimsingi za wamama wajawazito na watoto wachanga pamoja na watoto. Katika kambi nyingi za wakimbizi, hali inakuwa ni tofauti na ilivyokuwa katika makazi yao, na hivyo kusababisha ugumu wa maisha kwa wakimbizi hao. Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tutaangalia athari za vita na machafuko kwa wakimbizi wanawake na watoto.