Rais Xi asisitiza umuhimu wa kuharakisha kujenga mfumo wa kisasa wa viwanda
2023-05-05 22:16:20| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa mfumo wa kisasa wa uchumi unaojikita kwenye uchumi halisi.

Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati ya kijeshi, amesema hayo kwenye mkutano wa kamati kuu ya mambo ya fedha na uchumi ambayo pia yeye ni mwenyekiti.