Tatizo la saratani ya matiti kwa wanawake na jinsi ya kukabiliana nalo
2023-05-26 10:59:41| CRI

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wa kawaida au uliozidi kiwango, Kwahyo basi, Saratani ya matiti ni ugonjwa unaohusisha ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la titi au matiti. Ugonjwa huu huwa unatokea kwa wanawake n ahata wanaume pia. Hata hivyo saratani ya matiti kwa wanaume hutokea kwa nadra sana.

Hakuna mtu anayejua sababu halisi ya saratani ya matiti. Mara nyingi madaktari hawawezi kueleza kwa nini mwanamke mmoja anapata saratani ya matiti na mwingine hapati. Madaktari wanajua kuwa kujigonga, kujigusa, kujikwaruza au kushikashika au kunyonywa matiti hakusababishi saratani hii. Na kikubwa ni kwamba saratani ya matiti haiambukizwi.

Hata hivyo tafiti zinaonesha kuwa, wanawake fulani wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti kuliko wengine, ambapo kuna sababu kadhaa zinazoongeza hatari ya kupata saratani hii. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2020 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), wanawake wenye saratani ya matiti ni zaidi ya milioni 2.2 duniani, na inakadiriwa kuwa mwanamke mmoja kati ya 12 atapatwa na saratani ya matiti katika maisha yake na ndiyo chanzo kikuu cha vifo miongoni mwao. Hivyo leo katika kipindi cha ukumbi wa wanawake tutazungumzia tatizo la saratani ya matiti kwa wanawake na jinsi ya kukabiliana nalo.