Watu saba wauawa na wengine 22 kutekwa nyara nchini Nigeria
2023-05-08 18:59:29| cri

Watu saba wameuawa na wengine 22 wametekwa nyara katika mashambulizi mawili tofauti yaliyotokea katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Alhamis iliyopita, wakulima watatu waliuawa na wengine 11 kutekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la Islamic State West Africa Province (ISWAP), karibu na kijiji cha Bulayobe. Wakulima hao, waliingia kilomita 10 nje ya Banki kwa lengo la kusafisha mashamba kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kilimo kabla ya msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.