Biden atoa amri ya kupandisha bendera nusu mlingoti baada ya shambulizi la bunduki la Texas
2023-05-08 09:50:40| CRI

Habari kutoka Ikulu ya Marekani imesema, Rais Joe Biden ametoa amri ya kupandisha bendera nusu mlingoti baada ya shambulizi la bunduki lililotokea jimboni Texas.

Mashambulizi matatu mfululizo yalitokea Ijumaa na Jumamosi nchini Marekani, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 11 na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulizi moja lilitokea katika soko kubwa jimboni Texas Jumamosi mchana na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine saba kujeruhiwa. Jingine lilitokea Jumamosi alfajiri katika sherehe iliyofanyika nyumbani jimboni California, ambapo msichana mmoja aliuawa na wengine watano kujeruhiwa. Aidha katika shambulizi la tatu lililotokea Ijumaa usiku katika mgahawa ulioko jimboni Mississippi, limesababisha mtu mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa.

Biden alitoa taarifa akisema Ikulu ya Marekani inafuatilia kwa makini hali ya mashambulizi, na kuwasiliana na idara ya utekelezaji wa sheria na maofisa wa mikoa ili kutoa msaada.