Rais wa China akutana na wajumbe wa Mkutano wa 10 wa Urafiki wa Jumuiya za Wachina Wanaoishi Ng'ambo
2023-05-08 15:57:12| cri

Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi amekutana na wajumbe wa Mkutano wa 10 wa Urafiki wa Jumuiya za Wachina Wanaoishi Ng’ambo kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Umma mjini Beijing.

Rais Xi aliwakaribisha wajumbe hao na kutoa salamu kwa Wachina wote wanaoishi nje ya nchi kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China.

Mkutano wa Urafiki wa Jumuiya za Wachina Wanaoishi Nga’ambo ni jukwaa muhimu la kukuza urafiki kati ya jumuiya hizo kote duniani. Mkutano huu wa kumi wenye kauli mbiu ya "Kuunganisha China na Nchi za Nje, Kusukuma Mbele Ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja", umehudhuriwa na viongozi 500 wa jumuiya za Wachina wanaoishi katika nchi na sehemu zaidi ya 130 duniani.